Zaburi 93
Mungu Mfalme
1 Bwana anatawala, amejivika utukufu;
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwako tangu milele.
3 Bahari zimeinua, Ee Bwana ,
bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.
4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
5 Ee Bwana , sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako