Zaburi 41
Maombi Ya Mtu Mgonjwa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge,
2 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake,
atambariki katika nchi
na hatamwacha katika tamaa ya adui zake.
3 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani,
atamwinua kutoka kitandani mwake.
4 Nilisema, “Ee Bwana nihurumie,
niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.”
5 Adui zangu wanasema kwa hila,
“Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.”
6 Kila anapokuja mtu kunitazama,
huzungumza uongo,
huku moyo wake hukusanya masingizio;
kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.
7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,
hao huniwazia mabaya sana, wakisema,
8 “Ugonjwa mbaya sana umempata,
kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”
9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini,
yule aliyekula chakula changu
ameniinulia kisigino chake.
10 Lakini wewe, Ee Bwana , nihurumie,
ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.
11 Najua kwamba wapendezwa nami,
kwa kuwa adui yangu hanishindi.
12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza
na kuniweka kwenye uwepo wako milele.
13 Msifuni Bwana , Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele.