Zaburi 29
Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba
Zaburi ya Daudi.
1 Mpeni Bwana , enyi mashujaa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
2 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
3 Sauti ya Bwana iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
4 Sauti ya Bwana ina nguvu;
sauti ya Bwana ni tukufu.
5 Sauti ya Bwana huvunja mierezi;
mierezi ya Lebanoni.
6 Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni[~1~] urukaruke kama mwana nyati.
7 Sauti ya Bwana hupiga kwa miali
ya umeme wa radi.
8 Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;
9 Sauti ya Bwana huzalisha ayala,
na huuacha msitu wazi.
Hekaluni mwake wote wasema,
“Utukufu!”
10 Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;
11 Bwana huwapa watu wake nguvu;
*Zaburi 29:6 Yaani Mlima Hermoni.