1 Basi viongozi wa watu walikaa Yerusalemu, nao watu wale wengine walipiga kura ili kuleta mtu mmoja kati ya watu kumi aje kuishi Yerusalemu, mji mtakatifu, nao wengine tisa waliobaki wakae katika miji yao wenyewe. 2 Watu waliwasifu wale wote waliojitolea kuishi Yerusalemu.
3 Hawa ndio viongozi wa majimbo waliokuja kuishi Yerusalemu (baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi, watumishi wa Hekalu,[a] na wazao wa watumishi wa Solomoni waliendelea kuishi katika miji ya Yuda, kila mmoja katika milki yake mwenyewe katika miji mbalimbali, 4 ambapo watu wengine kutoka Yuda na Benyamini waliishi Yerusalemu).
20 Waisraeli waliosalia, pamoja na makuhani na Walawi, walikuwa katika miji yote ya Yuda, kila mmoja katika urithi wa baba yake.
21 Watumishi wa Hekalu waliishi katika kilima cha Ofeli. Siha na Gishpa walikuwa wasimamizi wao.
22 Afisa mkuu wa Walawi huko Yerusalemu alikuwa Uzi mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika. Uzi alikuwa mmoja wa wazao wa Asafu, waliokuwa waimbaji wenye kuwajibika kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu. 23 Waimbaji walikuwa chini ya amri za mfalme, ambazo pia ziliratibu shughuli zao za kila siku.
24 Pethahia mwana wa Meshezabeli, mmoja wa wazao wa Zera mwana wa Yuda, alikuwa mwakilishi wa mfalme katika mambo yote kuhusu mahusiano na watu.
25 Kuhusu vijiji na mashamba yake, baadhi ya watu wa Yuda waliishi Kiriath-Arba na makazi yaliyokizunguka, katika Diboni na makazi yake, katika Yekabzeeli na vijiji vyake, 26 katika Yeshua, katika Molada, katika Beth-Peleti, 27 katika Hasar-Shuali, katika Beer-Sheba na makazi yake, 28 katika Siklagi, katika Mekona na makazi yake, 29 katika En-Rimoni, katika Sora, katika Yarmuthi, 30 Zanoa, Adulamu na vijiji vyake, katika Lakishi na mashamba yake, na katika Azeka na makazi yake. Hivyo walikuwa wakiishi kuanzia Beer-Sheba mpaka Bonde la Hinomu.
31 Wazao wa Wabenyamini kutoka Geba waliishi Mikmashi, Aiya, Betheli na makazi yake, 32 katika Anathothi, Nobu na Anania, 33 katika Hazori, Rama na Gitaimu, 34 katika Hadidi, Seboimu na Nebalati, 35 katika Lodi na Ono, na katika Bonde la Mafundi.
36 Baadhi ya makundi ya Walawi wa Yuda waliishi huko Benyamini.
<- Nehemia 10Nehemia 12 ->-
a Yaani Wanethini (pia 11:21).